Shirika lisilo la kiserikali la Demmy Harmony Foundation (DHF) limefanikiwa kufika katika shule ya Sekondari Kigera iliyoko Kata ya Nyakatende, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara na kuzungumza na walimu wanaojitolea shuleni hapo pamoja na kuwaeleza malengo na nia ya shirika Hilo kwa walimu wanaojitolea nchini.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Demitria Gibure, amesema kufika Katika Shule hiyo ni Utekelezaji Majukumu mara baada ya uzinduzi Lengo ikiwa ni kuwafikia wafanyakazi hususani waliopo katika kada ya elimu, ili kuitambulisha kwa walengwa waweze kufahamu jinsi inavyotekeleza majukumu yake kupitia wazo la tabasamu na mwalimu, ambalo linahusisha kuwawezesha walimu kwa kuboresha maendeleo yao ya kitaaluma, ustawi na kutambuliwa na kuhakikisha kuwa wana vifaa vya kufikia matokeo mazuri kwa jamii
"Tunaendelea na utekelezaji wa majukumu yetu kwa walengwa hususani waliopo kwenye mikoa ambayo wameanza utekelezaji wa majukumu ambayo ni mikoa ya Pwani, Dar es Salaam,Tanga,Njombe, Mwanza,Mara,Singida na Mtwara" Amesema Demmy
Shirika la Demmy Harmony Foundation limeanzishwa na mwanaharakati na mjuzi wa lugha ya Kikwaya, Kiswahili na Kiingereza Demitria Gibure, likiwa na dira ya kuwezesha na kuinua taaluma ya ualimu nchini Tanzania, kwa kurejesha thamani yake na kukuza matokeo chanya katika elimu huku likiwa na dhamira ya kuimarisha maendeleo ya kitaaluma, kutambuliwa, na ustawi wa walimu nchini Tanzania, kutetea fidia ya haki na maendeleo ya taaluma huku ikishirikiana na wadau kuboresha ubora wa elimu kwa manufaa ya jamii.
Katika kipindi kifupi tangu kuanzishwa kwake shirika la Demmy Harmony Foundation, limefanikiwa kuwaunganisha walimu na wadau wengine wa elimu ndani na nje ya nchi ya Tanzania pamoja na kufikisha la tabasamu na mwalimu kwa njia mbalimbali kama vile kutumia vyombo vya habari kama vile Runinga na Redio, pia kupitia mitandao ya kijamii.