Maafisa Lishe, Afya na Biashara Mkoa Kigoma Wapatiwa Mafunzo ya Afya ya Urutubishaji wa Chakula

0


Maafisa Lishe, Afya na Biashara Mkoa wa Kigoma Wapatiwa Mafunzo ya Usimamizi wa Afua ya Urutubishaji wa Chakula

Maafisa lishe, afya na biashara kutoka halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Kigoma wamepatiwa  mafunzo maalum juu ya usimamizi na ufuatiliaji wa afua ya urutubishaji wa chakula. Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wa kusimamia wasindikaji wa bidhaa za chakula zilizoongezwa virutubishi muhimu, kama sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kupambana na tatizo la lishe duni nchini.

Katika mafunzo hayo, washiriki wamepitia rasimu ya mwongozo wa utekelezaji wa afua ya urutubishaji, wakitoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia katika kuandaa mwongozo wa kitaifa wa urutubishaji wa chakula. 

Mwongozo huu unatarajiwa kutoa mwongozo wa wazi kwa utekelezaji wa afua hiyo kwa kushirikisha sekta zote na idara zilizoko chini ya mamlaka za serikali za mitaa, pamoja na wadau wa maendeleo na sekta binafsi katika maeneo husika.

Uandaaji wa mwongozo huu unafuata mbinu ya bottom-up approach – yaani kuanzia kwa watekelezaji wa chini hadi kwa watunga sera – ili kuongeza umiliki wa afua hii ngazi ya jamii (localization) na kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa rahisi na wenye ufanisi mkubwa.

Mafunzo haya yanaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Viwanda na Biashara, pamoja na kampuni ya Sanku, ambayo ni mmoja wa wadau wakuu wanaojihusisha na urutubishaji wa chakula nchini.

Mafunzo hayo ni utekelezaji wa maelekezo ya Wizara ya Viwanda na Biashara, yanayolenga kuhakikisha kuwa mazingira rafiki kwa utekelezaji wa afua ya urutubishaji yanaandaliwa mapema, ili ifikapo Desemba 2025, kanuni za urutubishaji wa chakula ziweze kutumika kikamilifu nchi nzima.

#NFNC Tanzania





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top