Ubalozi wa Ujerumani Nchini Tanzania umetangaza fursa Kwa wasanii wa Sanaa za Kuona wa kitanzania.
Mpango wa Kimataifa wa Sanaa wa Leipzig (LIA) nchini Ujerumani unatoa nafasi za usanii wa miezi 3 ikiwa imegharamiwa kikamilifu jijini Leipzig kuanzia Novemba 3, 2025 hadi Januari 29, 2026!
🎨 Kaulimbiu: Tafakari juu ya historia na umuhimu wa sasa wa wamisionari wa Herrnhut (Kanisa la Moravian) nchini Tanzania.
Kinachojumuishwa:
🏡 Chumba cha bure chenye ukubwa wa mita za mraba 83 ikiwa na samani
💶 Ufadhili wa €800 kwa mwezi
✈️ Gharama za usafiri, viza na bima ya afya zitalipiwa
🧠 Msaada wa kitaalamu kutoka kwa wasimamizi wa sanaa
🖼️ Maonesho ya pamoja wakati wa Spinnerei Rundgang (Januari 2026)
Sifa za Muombaji:
✅ Awe anaishi Tanzania
✅ Awe na uelewa mzuri wa lugha ya Kiingereza
✅ Mradi uhusishe historia ya Tanzania na Ujerumani
📅 Mwisho wa kutuma maombi: 22 Juni 2025, saa 6:00 mchana CET
📧 Tuma maombi (PDF moja) kwa: marina.diaz@liap.eu & assistent@liap.eu
✉️ Kichwa cha barua pepe: Open Call Tanzania
🔗 Maelezo zaidi: https://liap.eu/index.php/en/application/