SMAUJATA Mara Yatoa Elimu ya Ukatili wa Kijinsia Kwa Wanafunzi na Wazazi Songambele

0


 

Na Shomari Binda-Musoma

ELIMU ya masuala ya ukatili wa kijinsia na masuala ya maadili kwa wanafunzi imeendelea kutolewa na viongozi wa Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii ( SMAUJATA) mkoa wa Mara kwa kushirikiana na viongozi wa Wilaya ya Musoma.

Kupitia kampeni hiyo inayolenga Lkutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia Katika Mkoa WA Mara, imefanikiwa kuwafikia Wazazi na wanafunzi wa shule ya msingi Songambele Mei 30,2025  kwa kuwezeshwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Musoma kupitia Katibu Tawala Ally Mwenda.

Awali akizungumza kwenye kikao cha wazazi wa shule ya Songambele wakati  akitoa Elimu hiyo Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Mara Joyce James Ngasa ametoa wito Kwa wazazi kutowaacha watoto kujilea wenyewe majumbani bila usadizi wa Wazazi na walezi.

Amesema malezi Bora  ya watoto yanaanzia nyumbani kwa uangalizi mzuri wa watoto na kazi ya kulea wasiachiwe walimu pekee yao.

Joyce amesema kwa sasa mmomonyoko wa maadili umekuwa mkubwa, hali iliyopelekea SMAUJATA mkoa wa Mara na Wilaya ya Musoma kupita mashuleni kutoa elimu Kwa wanafunzi, Wazazi na walezi

Amesema wazazi na walezi wanapaswa kutimiza wajibu wao kwa kuzungumza na watoto na kuwaelekeza maadili mema na kutowafanyia ukatili wa aina yoyote.

Baada ya kuzungumza na wazazi Mwenyekiti huyo alizungumza na na wanafunzi wa shule ya msingi Songambele na kuwataka kutoa taarifa pale wanapofanyiwa vitendo vya ukatili vikiwemo vya ubakaji na ulawiti.

Amewaambia wanafunzi hao pale wanapofanyiwa vitendo vibaya kutoka kwa mtu yoyote ikiwa nyumbani au sehemu yoyote watoe taarifa.

" leo tumeendelea na utoaji wa elimu kwa kufika shule ya msingi Songambele na kuzungumza na wazazi pamoja na wanafunzi.

" Tumepokelewa vizuri na uongozi wa shule na tumewaelekeza wazazi juu ya kujiepusha na ukatili wa aina yoyote kwa watoto lakini pia tumezungumza na wanafunzi tunaamini kampeni na elimu hii italeta mabadiliko",amesema.

Aidha Mwenyekiti hiyo wa SMAUJATA mkoa wa Mara ameushukuru uongozi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kuwapa ushirikiano na kuwawezesha usafiri wa kufika mashuleni na kutoa elimu.

Kampeni ya utoaji elimu unaofanywa na SMAUJATA mkoa wa Mara inaendelea kwenye shule za msingi na sekondari Wilaya ya Musoma na baadae itaendelea kwenye Wilaya nyingine za mkoa wa Mara.

# Kataa Ukatili wewe ni Shujaa










Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top