Watendaji Watakao Bainika Kufanya Udanganifu Katika Daftari la Wakazi Kyerwa Kuchukuliwa Hatua

0


Na Angela Sebastian- Kyerwa

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Zaitun Msofe amewataka watendaji wa kata na vijiji kuakikisha wale wote wanaoandikishwa kwenye daftari la wakazi wawe ni Raia wa Tanzania pekee  uku akisema kuwa atakayeandikisha mtu asiye raia wa Tanzania kwa maslai  yake binafsi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake

Msofe amesema kuwa serikali imeanzisha zoezi hilo ili kuwatambua wenyeji na wageni wanaishi katika Wilaya hiyo kwa utaratibu maalumu ikiwa na   lengo  la kulinda usalama wa Wilaya hiyo na wananchi wake.

Msofe ametoa agizo hilo leo katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri  hiyo ambacho kimejadili taarifa  ya utekelezaji ya miradi ya maendeleo kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo,amesema uandikishaji huo ni nguzo muhimu ya kuimarisha ulinzi na usalama wa Wilaya hiyo na nchi kwasababu  Wilaya hiyo iko mpakani.

Wakati huohuo baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo wametoa wiki moja kwa wazazi wote ambao hawajapeleka watoto wao waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza kuripoti shuleni   kuhakikisha wanawapeleka shule hata kama hawana sare za shule uku wakisema kuwa baada ya wiki moja msako mkubwa wa kuwakamata wazazi hao utaaanza rasmi na hatua kali za  kisheria zitachukuliwa .










Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top